habari tulizozipata hivi punde ambazo pia zimethibitishwa na wanafamilia ya Askofu Dk Moses Kulola ni kwamba, askofu huyo wa kanisa la E A G T Ametangulia kwa Bwana leo hii.
Katika mitandao ya kijamii, wengi wametoa maoni yao kuhusu kifo cha Moses Kulola
Askofu Kulola ni
'Mtumishi
wa Mungu mwenye moyo wa Uinjilisti, Aliyefanya kazi kwa muda mrefu tena
kwa UAMINIFU MKUBWA, akizunguka huku na kule Tanzania na nchi zingine
akibeba habari njema na nzito za Injili ...aliyekubali mateso kwa ajili
ya Injili....aliyezaa matunda mengi kiroho....Ninayemheshimu sana
....hata nilipokuwa mdogo niliwahi kuota kuhusu yeye....alihusisha mambo
mengi na Injili ....hata watu waliookoka chini yake aliwaita wana wa
Injili...Binafsi Yesu alikuwa Rafiki wa pekee kwake....hata cheo cha U
dokta hakitoshi kwake ...bado amekuwa mnyenyekevu wa moyo, mwenye huruma
sana kwa wanaoteseka ....mkali sana kwa mapepo na nguvu za
giza...aiyeogopa kukemea Injili za aina nyingine zinazotaka kutoka
kwenye msingi wa injili halisi....Ninamependa sana sana ....sasa ni nini
hiki naanza kusikia watu wanasema' (Abel Orgenes)
'Naomba Isiwe Kweli ..... Vita Amevipiga, Imani Ameilinda na Mwendo ameumaliza.....' (Samwel Sasali)
'R. I. P. lev moses kolola pumzika kwa amani baba yetu wa kiloho.nipengo kubwa kwa watanzania' (Ballack Alberto)
Wengi wametoa masikitiko yao, lakini cha muhimu ni kwamba AMEMTUMIKIA MUNGU KWA UAMINIFU WOTE, tunaamini kuwa amepumzika ba siku ya Mwisho tutamlaki Yesu Kristo pamoja mawinguni tusipozimia mioyo.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMEN
No comments:
Post a Comment