MPANGO
WA MAANGAMIZI
DHAMIRA NA DHAMBI
Jifunze
John ni kijana aliyejiunga na kanisa
hivi karibuni, katika kipindi cha wiki mbili hivi ambazo amefika kanisani, ana
bidii sana katika mambo ya Mungu. Ni mwombaji, ana nena kwa ligha na mwimbaji
ambaye anonekana maarufu sana. Diana amevutiwa naye sana, hata kama hamfahamu
vizuri. John pia naye anonyesha kuvutiwa na Diana, na angependa kumchumbia. Je,
ni halali kwao kuanza uchumba
Jifunze
Sarah ni msichana mabaye hajaokoka.
Sengi ni mvulana aliyeokoka na amemwona Sarah. Ameonyesha nia ya kumwoa na
wamekubaliana Sara ajiunge na kanisa anakoabudu Sengi. Sarah amejiunga, ametubu
na ameokoka. Je, ni vema kuendelea na uchumba?
Mstari wa kukumbuka:
Njia
zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho (motive/dhamira) za watu (Mithali 16:2)
Bali
ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye
atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo;
ndipo kila mtu ataipata sifa yake kwa Mungu (1Wakorintho 4:5)
1. DHAMIRA
Tunapifikilia kila hali
ni vema kuangalia matokeo yake katika uhalisia na kuziaangalia dhamira za mioyo yetu. Thamira zetu lazima
ziwe safi.
Jiulize: Nini kinachomsukuma kijana/msichana anayetaka kuoa/kuolewa na
asiyeokoka?
- Ni kwa sababu anahitaji amrejeshe kwa Kristo kupitia uhusiano huo?
- Je, ni kwa sababu ni mzuri?
- Ni kwa sababu anataka kuoa/kuolewa?
- Ni kwa sababu anafikiri ataokoka mbele ya safari?
- Ni uasi kwa wazazi wake?
- Ni uasi kwa kanisa?
- Ni uasi kwa Mungu?
- Ni kwa sababu ya mashindano, hitaji la mwenzi au msukumo wa rika (peer pressure)?
- Wana muda wa kuhabarishana kuhusu wokovu wa Yesu au wataongea kuhusu mahusiano yao na maisha ya baadaye
- Chanzo/msukumo wa mahusiano haya ni Yesu ndai yao au ni uhusiano wao wenyewe?
UKWELI
- Jambo muhimu sio sisi tunataka nini, bali ni Mungu anataka nini.
- Upendo halisi husubiri
- Upendo halisi unapimwa kwa kutoa na si kupokea
- Upendo halisi unapima matokeo ya mbele kuliko ya sasa
- Upendo upo tayari kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya wengine
- Kama unaona dalili zozote za udhaifu katika mahusiano hayo, kwanini uendelee? Huo si upendo, bali ni tamaa
2. DHAMBI
Chanzo cha Anguko -Dhambi (Mwanzo 3:1-6)
Katika mistari hii
tunaona tatizo liliopelekea anguko la mwanadamu wa kwanza na mabazo ni chanzo
cha anguko la wanadamu wote.
V1-Nyoka (shetani) sio mjinga kama wengi wanavyofikiri; ni mwerevu
na mjanja kuliko wanyama wote wa mwituni (sio mwerevu kuliko mwanadamu, kwani
mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu; hivyo shetani hawezi kuwa mwerevu kuliko
Mungu).
V1:- Shetani ni mwongo. Ili kumwangusha mwanadamu huongeza/
kupunguza au kubadili Neno la Mungu. Alitumia neno ‘ati’ halafu akaendelea
kupotosha maagizo ya Mungu kwa mwanadamu. Hii ni silaha aitumiayo hadi sasa.
Mf: kijana anamwambia binti, ‘kama’ unanipenda …. Huu ni uongo. Upendo hauna
masharti, ni ukweli.
V2-5: Eva aliingia katika mtego kwa kukubali kufanya mazungumzo na
shetani. Kwa kuwa hakuna urafiki katika ya nuru na giza, pia hakuna mapatano
kati ya shetani na mwana wa Mungu. Ukiruhusu mazungumzo, basi utajikuta
unaingia mtegoni. Nyakati Fulani mwanadamu anapokemea mapepo na kuyaruhusu
kusema, huchonganisha watu. Usimruhusu shetani.
V6:- Mwanamke alipoona ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza
macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi ailitwaa katika matunda
yake akala, akampa mumewe naye akala. (Mwanzo 3:6). Katika mstari huu
tunajifunza kuwa anguko la mwanadamu yeyote husababishwa na:
- Vitu vinavyoonekana kwa macho
- Vitu ambavyo kwa mtazamo wa kibinadamu ni kwamba vinafaa
- Vitu vinavyopendeza moyo wa mwanadamu
- Tamaa ya kupata vitu Fulani
- Na hitaji la kutaka kujua (hasa vitu vipya)
Angalia: 2Samweli 11:1-4. Daudi alijaribiwaje?
- Aliamua kutoenda vitani, akapumzika tu. Hii ilimweka katika hali iliyompelekea kujaribiwa
- Alimwona Bathsheba na jaribu lilianza alioendelea kumwangalia
- Alichukua hatua ya kuzini naye
Angalia: Mwanzo 39:4-12 Yusufu alishindaje jaribu?
- Alikuwa makini na kazi zake (was busy with work)
- Mke wa Potifa alipomjaribu alikataa
- Mke wa Potifa alipomkamata kwa lazima, alikimbia.
TUNACHOJIFUNZA
Mtego wa shetani huonekana unafaa wakati unaanza, lakini
mwisho wake unalipa gharama kubwa sana kwa matokeo ya yale uliyofanya kama
hautamkataa.
Vijana wengi wameanguka kwa
sababu wamekuwa hawajishughulishi, hupenda maisha ya raha. Hudhani wanaenda na
wakati. Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinaonekana si vibaya kufanya lakini
vimekuwa vikiwapelekea kuanguka, mfano:
- Kusalimiana kwa mikono
- Kupeana busu
- Kupeana
zawadi
- Kuwa pamoja kwa chakula cha machana/jioni (out)
- Kuhudumu pamoja wakiwa pea sawasawa (1+1, 2+2 au hata 5+5) za jinsia.
KUMBUKA:
Njia
zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho (motive/dhamira) za watu (Mithali 16:2)
<<<<<<<<<<<<<<
PRAY >>>>>>>>>>>>>>
No comments:
Post a Comment