UTANGULIZI
Mpango wa Mungu kwa mwanadamu ni wa ajabu sana, haufungwi na muda au
mahali ambao ukifuatwa kwa uaiminifu na ukamilifu, utimilifu wake si wa mashaka
hata kidogo. Hata hivyo, Mungu angependa ushiriki katika mafanikio yako ili uwe
sehemu ya mafanikio yako kama ilivyokuwa katika
Yohana 11:39, ambapo Yesu aliwataka ndugu wa Lazaro (aliyekufa), washiriki
katika muujiza wa kufufuka kwa Lazaro kwa kuliondoa jiwe
UTII
Ili Mungu
amwage baraka juu ya maisha yako, unahitaji kuwa mtii kwa Neno lake (Kumb
28:2). Kwa hakika, kutii Neno la Mungu ni muhimu katika mafanikio yako kiuchumi
(Yoshua 1:8)
Mafanikio
ya maisha yako ya mbele kiuchumi yana uhusiano wa moja kwa moja na jinsi
unavyotii kanuni za Mungu kuhusu utoaji. Unahitaji kushiriki katika muujiza
wako, Neno la Mungu linaagiza kumheshimu BWANA kwa mali zetu ili tupate mavuno mengi
maishani (Mithali 3:9-10).
AHADI
Mungu
anataka kukubariki katika kila eneo la maisha yako, ikiwa ni pamoja na hali
yako ya uchumi. Kumbuka tunaposema uchumi ni fedha na mali nyingine kama mifugo, mashamba,n.k. Hivyo, Mungu anapenda upate
fedha na mali
ili uvitumie kwa utukufua wake.
1. Hakuna kizuizi chochote cha baraka za Mungu kwa sababu vyote ni mali yake na
haviwezi kuisha kwani yeye ndiye aliyeviweka (Wafilipi 4:19)
2. Baraka za Mungu zitaendelea kukufuata wewe na watoto wako (Zaburi
115:14).
3. Mungu atakufundisha jinsi ya kufanikiwa (Isaya 48:17).
4. Mungu atabariki kazi za mikono yako (Kumb. 28:12)
5. Mungu atakuwezesha kufanikiwa (Kumb 8:18)
6. Kwa jinsi unavyozidi kumtafuta, Mungu atakutana na mahitaji yako (Zaburi
24:10)
7. Ikiwa utamtii na kumheshimu, Mungu atakubariki wewe na jamaa yako
(Zaburi 112:1-3)
8. Baraka za Mungu kwako ni njema wakati wote (Mithali 10:22)
9. Mungu ataubariki uaminifu wako (Mithali 28:20)
10. Unapowapa wahitaji, Mungu naye atakutana na mahitaji yako;
Hautapungukiwa kamwe (Mithali 28:27)
11. Ukitoa kwa moyo mkunjufu, Mungu atakumwagia baraka tele (2Wakorintho
9:6-7)
12. Unaweza kufungulia baraka za Mungu maishani mwako leo iwapo utamtii Mungu
katika maeneo ya utoaji. Baraka katika utoaji ni mfano wa kupanda mbegu. Biblia
inasema kila mtu apandacho ndicho atakachovuna (Wagalatia 6:7). Ukitoa
kitu/vitu dhaifu tegemea kupokea kidogo. Angalia mfano wa Kaini na Habili
(Mwanzo sura ya Nne).
Sijaona
mkulima ambaye anapanda bila ya kutegemea kuvuna. Pia wakati wa mavuno, mkulima
mwenye busara huweka mbegu/hupanda mbegu kwaajili ya mvuno mengine, wakati
ziada ikitumiwa kukidhi mahitaji yake binafsi. Hii ndio kanuni ya mafanikio, na
Mungu ameahidi katika hili (Luka 6:38)
UNACHOHITAJI NI MBEGU
Wakati
Mungu ndiye atoaye mavuno, mimi na wewe tunahitaji kupanda mbegu. Huu ni wajibu
wetu.
Kanuni Saba Za
Mavuno
1. Lazima mbegu ipandwe ili kutoa mavuno (Yohana 12:24). Mbegu
inayozaa lazima kwanza ipandwe, hata kama
mbegu inaweza kuonekana ndogo mikononi mwa mkulima, lakini unapoipanda unakua
umeachilia uwezo wake wa kuzaa mtunda mengi.
2. Mbegu
lazima ihuishwe (Yohana 12:24)
Mavuno yaliomo ndani ya mbegu yamefichwa hadi mbegu
ihuishwe.. Wakati mbegu ikiwa imehuishwa huonekana haifai kwa matumizi yoyote.
Baada ya muda huu ndipo mbegu inaota na kukua tayari kwa mavuno. Kumbuka
unapopanda mbegu katika kazi ya Mungu, inakua haifai kwa matumizi yako binafsi,
lakini inahifadhiwa na kuzidishwa. Baada ya kuzidishwa inarudi kwako kwaajili
ya mavuno.
3. Panda
kile unachotegemea kuvuna (Mwanzo 1:12)
Ukipanda maharage hauwezi kuvuna mpunga, vivyo
hivyo kwa kila mbegu upandayo. Kwa kuzingatia kanuni ya kupanda na kuvuna,
utavuna mazao ya aina ya mbegu uliyopanda.
4. Kiasi
cha mavuno kinategemea kiasi cha mbegu ulizopanda (2Wakorintho 9:6). Mungu hawezi kukupangia kiasi utakachovuna, wewe mwenyewe unahitaji
kukipanga kwa kujua kiasi kipi upande na uvune kiasi gani. Mkulima apandaye
heka tano (5) za mpunga atapata mavuno zaidi kuliko aliyepanda nusu heka (0.5).
5. Panda
kwenye udongo mzuri, wenye unyevu (Mathayo 13:3,8). Mbegu lazima ipandwe kwenye udongo mzuri ili iote na kutoa mvuno
mazuri.. udogo mzuri ni wenye rutuba, ulioandaliwa vizuri, wenye kasi cha maji
cha kutosha tayari kupokea mbegu.
6. Mavuno
huja baada ya kusubiri kwa muda (Marko 4:26-2)
Inachukua muda kupanda mbegu, kuota, kukua hadi
kufikia mavuno. Nguvu ya mavuno inatokea taratibu jinsi mmea unapokua, na
wakati fulani unaweza kuona kuwa mazao yangu yatatoa mavuno mengi.
7. Lazima
shamba litunzwe ili kutoa mavuno (Mathayo 13:3,7) Mbegu iliyopandwa lazima itunzwe vizuri ili kutoa mavuno. Inahitaji maji
ya kutosha, magugu yatolewe, palizi lifanyike kwa wakati ili kuruhusu mbegu
kukua kwa afya njema na itoe mavuno mengi na mazuri.
Unapopanda
mbegu katika Bwana, unapanda kwa imani na kuondoa magugu kwa njia ya maombi na
kumsifu Mungu.
KUMBUKA
1. Usile
mbegu Watu wengine wenye mahitaji wamesahau na kufanya
makosa kwa kula mbegu badala ya kupanda. Ni mbegu iliyopanwa pekee ndiyo inweza
kuzaa mavuno mengi
2. Endelea kupanda mbegu Usiache kupanda mbegu ili kupata mavuno mengi (Mhubiri 11:6)
HITIMISHO
Kupanda ni
kanuni ya mbinguni, kanuni iliyowekwa na Muumbaji Mwenyewe. Kama
mkulima yeyoye anavyopanda mbegu ardhini akitarajia mavuno, kwa hiyo kanuni hii
itamsaidia yeyote anayetaka kufanikiwa kiuchumi kama
ataitumia kwa uaminifu. Ni rahisi, panda
mbegu, vuna mavuno. Kumbuka, siri ya mavuno yako ipo katika mbegu.
MBEGU NI NINI?
Matoleo ya
aina yoyote kama vile:
Sadaka, Kikumi, Uaminifu, Kuwaona wenye shida,
Kusaidia wenye shida, Kutmbelea
wahitaji, Kuwapenda wengine n.k
PANDA MBEGU LEO
No comments:
Post a Comment